PEPO UBATIZO

BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI nawasalimu watu wote wa mataifa yote katika jina lililo juu kuliko yote hapa ulimwenguni la YESU mwana wa MUNGU wa pekee. Karibu katika somo la kufunguliwa uujue ukweli kuhusu ubatizo mtakatifu na ubatizo wa kipepo na ambao unatumika katika sehemu nyingi katika nchi zote duniani na watu hawajui kuwa ubatizo huo siyo ubatizo wa kipepo ila watu wanabatizwa katika sehemu baadhi wakijua ni ubatizo mtakatifu kwa sababu linatajwa jina la MUNGU BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU na kumbe ni kinyume na ubatizo mtakatifu. Ila zaidi ili uelewe ubatizo mtakatifu na wa kweli soma katika mafundisho niliyofundishwa na YESU katika blog hii na hata vitabu nilivyoviandika mimi Nabii Hebron vitakuweka huru na siku moja utafika mbinguni kwa ajili ya kuujua ukweli na ukaufwata sawa sawa na neno la MUNGU lilivyoandikwa katika kitabu cha biblia. Ninaposema pepo ubatizo ninamaanisha huyu ni roho mchafu wa shetani ambaye ametumwa na shetani kuuleta ubatizo wa uwongo na ukatumika katika makanisa badala ya kufwatwa ule ubatizo aliobatizwa YESU pale Yordan, utaona na ROHO MTAKATIFU alishuka kushuhudia ubatizo mtakatifu. Hivyo mpaka sasa umeelewa kuhusu ubatizo mtakatifu na ule ambao YESU aliobatizwa na maji mengi katika mto. Sasa shetani na yeye akamleta roho wake mchafu asimamie batizo za uwongo ambazo ni batizo zote ambazo hazipo katika biblia, katika biblia upo ubatizo mmoja wa Yohana peke yake na YESU ndio aliobatizwa. Sasa tofauti na ubatizo ule wa maji mengi nataka uelewe batizo hizo zinasimamiwa na pepo batizo na ukiwa unabatizwa batizo za jinsi hizo uelewe na wewe unabatizwa ubatizo wa kipepo na hata anayebatiza batizo hizo aelewe anabatiza batizo za kipepo na siyo batizo za ROHO MTAKATIFU. Japo najua hata watumishi wengi hawajui jambo hili ila wapo wengi wanajua kabisa wao ni watumishi wa shetani na baba yao ni shetani na wanauendeleza ufalme wa shetani ili YESU wa kweli asiwapate hao watu kama ilivyo sasa, idadi kubwa ya watu wengi hawajabatizwa ubatizo mtakatifu, wamebatizwa ubatizo wa kipepo. Hivyo uamue ukabatizwe haraka ubatizo mtakatifu ili ile alama ya pepo ubatizo au 666 ikuondoke na uwe mwanafunzi wa YESU wa kweli. Amenituma YESU niwaeleze ukweli. Maneno hata alipokuwa ananieleza alikuwa anatoa machozi kwa ajili ya wanadamu wanavyompenda halafu hawaelezwi ukweli na wao wakijua wamempokea roho wake mtakatifu kumbe wamempokea pepo. Hii ni kwa sababu watumishi baadhi yao aliowatuma wamemsaliti na badala yake wameamua kuyasimamia mafundisho ya uwongo na kwa njia hiyo hata wale wote ambao wanaongozwa nao wamefanyika kuwa mateka ya shetani na YESU sasa anarudi. Embu tazama kila aliyewekewa ubatizo wa kipepo hata nyakuliwa kwa sababu anayo alama ya ubatizo wa kipepo. Ipo neema sasa uokoke na ubatizwe ubatizo wa kweli wa ROHO MTAKATIFU na huo ubatizo wa kipepo ukatoke katika jina la YESU. BATIZO ZA KIPEPO NI ZIPI? Ni batizo zote tofauti na ule wa Yohana mtakatifu na aliobatizwa YESU na akasema tuufwate huo. Batizo za kipepo ni za uwongo, hazijaandikwa hata katika kitabu kitakatifu, na hata biblia inasema katika kitabu cha Ufunuo 22:18-19; atakaye yaongeza au kuyapunguza maneno ya kitabu hiki hataenda mbinguni. Shetani alibuni njia nyingi ikiwemo hii ya ubatizo tofauti na wa biblia ili tu kukuteka wewe na wengine. Hata mimi nilishabatizwaga ila neema ya YESU ikanitoa, na wewe huu ndio wakati sasa. Ubatizo wa maji ya kikombe. Ubatizo wa watoto wadogo. Ubatizo wa maji ya kisima. Ubatizo wa ziwani. Ubatizo wa maji mengi halafu ukabatizwa kwa jina la mchungaji. Hizo zote hazipo katika katiba (biblia) kwa ajili ya kuwaongoza watu kwenda mbinguni. Sasa kama hazipo basi ujiulize swali je roho yupi huyo anayempinga MUNGU au kukataa kufwata ya MUNGU? Hata kulibadilisha neno lake? Huyo ndiye pepo ubatizo na kazi yake ni kuwawekea watu alama yake ya kipepo ili wanadamu wawe wa shetani. Nawaeleza myaelewe mrejeeni YESU, hata watumishi mlioiga mapokeo hayo pasipo kujua umeandaliwa moto kwa ajili ya watumishi ambao wamekubali kuzifanya kazi za pepo huyu ili kuimarisha ufalme wa shetani, tubuni sasa. Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu katika kitabu cha uzima wa milele naomba uniongoze nikabatizwe ubatizo wa ROHO MTAKATIFU na kama nilibatizwa wa kipepo unitoke katika jina la YESU. Amen. NABII HEBRON. Prophet Hebron http://prophethebron.blogspot.com/
Previous
Next Post »