Ufunuo wa Mbinguni na Kuzimu wa vijana 7

Ufunuo wa Kuzimu --- (Ushuhuda wa kwanza, Esau) --- 2 Wakorinto 12:2 : Namjua mtu mmoja katika Kristo,yapata sasa miaka kumi na minne-kwamba alikuwa katika mwili sijui;kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;Mungu anajua-mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Tulikuwa ndani ya chumba,wakati tulipo pata uzoefu huu wa kwanza.Chumba kilianza tena kujaa na utukufu wa Bwana. Ulikuwa na nguvu sana kiasi kwamba ulikiangazia chumba chote. Chumba kilikuwa kimejaa utukufu wake,ilikuwa ni jambo zuri kuwepo mbele zake. Yesu alituambia,"Watoto wangu wakiume,sasa nitawaonyesaho Ufalme wangu, tutakwenda kwenye utukufu wangu." Tulishikana mikono na tuliinuliwa juu. Nili angalia chini na niligundua kuwa tulikuwa tunatoka nje ya miili yetu. Tulipotoka nje ya miili yetu tulikuwa tumevaa mavazi meupe na tulianza kwenda juu kwa mwendo wa kasi sana.Tulifika mbele ya malango yaliyo fuatana ambayo ni njia ya kuingilia kwenye ufalme wa Mbinguni. Tulishangaa kile kilicho kuwa kina tutokea. Shukrani nyingi,Yesu mwana wa Mungu alikuwepo pale pamoja nasi, pamoja na malaika wawili ambao kila mmoja alikuwa na mabawa manne. Malaika walianza kuongea nasisi, lakini hatukuelewa kile walicho kuwa wanasema . Lugha yao ilikuwa tofauti sana na ile ya kwetu, haikufanana na lugha yeyote ile ya duniani. Malaika hawa walikuwa wakitukaribisha na waliifungua milango ile mikubwa sana. Tuliona eneo la ajabu sana, lenye vitu vingi tofauti tofauti. Tulipoingia ndani, amani ya kweli ilijaza miyoyo yetu. Bibilia inatuambia kuwa Mungu atatupa amani ipitayo fahamu za kibinadamu (Wafilipi 4:7) Kitu cha kwamza kukiona ilikuwa ni swala,hivyo nilimuuliza mmoja wapo wa marafiki zangu,"Sandra, je unaangalia kitu kile kile ninacho kiangalia?" hakuwa analia wala kupiga makelele tena, kama wakati ule tulipo onyeshwa kuzimu. Alikuwa akitabasamu na alisema:"Ndiyo Esau, ninamwaangalia Swala!" Hivyo nilijua kuwa kila kitu kilikuwa halisi, kweli tulikuwa kwenye Ufalme wa Mbinguni. Hofu zote ambazo tuliziona kule Kuzimu haraka zilikuwa zimesahaulika. Tulikuwa mahali pale tukiufurahia utukufu wa Mungu. Tulikwenda mahali pale ambapo Swala yule alikuwepo, nyuma yake ulisimama mti mkubwa sana! Ilikuwa ni katikati ya bustani. Bibilia inatuambia katikaUfunuo 2:7"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.Yeyey ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu" Mti huu ni ishara ya Yesu, kwasababu Yesu ni uzima wa milele. Nyuma ya ule mti kulikuwa na mto wenye maji angavu. Ulikuwa mweupe na mzuri sana, hatukwa tumewahi kuona tena kitu kama hiki duniani. Tulitaka tuu kubaki mahali pale. Mara nyingi tulimwambia Bwana,"Bwana tafadhali! Usitutoe mahali hapa! Tunataka kuwepo hapa milele! Hatutaki kurudi tena duniani Bwana alitujibu"Ni muhimu kwamba mrudi mkatoe ushuhuda wa kila kitu ambacho nimekiandaa kwa wote wale wanao nipenda, kwa sababu ninarudi mapema sana na ujira wangu u pamoja nami" Tulipo ona mto, tulifanya haraka na tukaingia ndani yake. Tulikumbuka msitari ule unao sema;Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena,mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.. (Yohana 7:38) Maji ndani ya mto huu yanaonekana yana uzima yenyewe, hivyo tulijizamisha wenyewe ndani yake. Ndani na nje ya yale maji tuliweza kupumua kawaida. Mto ule ulikuwa na kina kirefu sana na kulikuwa na samaki wa rangi tofauti wakiogelea ndani yake. Mwangaza ndani na nje ya maji ulikuwa wa kawaida; Mbinguni , mwanga hautoki kwenye kitu fulani,kila kitu kimetiwa mwangaza wake. Bibilia inatuambia kuwa Bwana Yesu (Ufunuo 21:23). Kwa mikono yetu, tulichukua baadhi ya samaki, nje ya maji, hawakufa. Hivyo tulimkimbilia Bwana na kumuuliza kwanini? Bwana alitabasamu na alijibu kwamba Mbinguni hakuna tena kifo, hakuna kilio tena, hakuna maumivu tena (Ufunuo 21:4) Tuli uacha ule mto na tulikimbia kila mahali tulipo weza, tulitaka kugusa na kuwa na uzoefu wa kila kitu. Tulitaka kurudi na kila kitu nyumbani kwa ababu tulishangazwa sana na vitu vya mbinguni. Kwa kifupi huwezi kuvielezea kwa maneno. Wakati Mtume Paulo alipochukuliwa Mbinguni, aliona vitu ambavyo hakuweza kuvielezea kwa maneno, kwa sababu ya uk..COPY LINK IFUATAYO KUPATA FULL STORYhttp://www.google.com/url?q=http://www.divinerevelations.info/documents/7_jovenes/swahili_7_columbian_youths_heaven_ufunuo_wa_mbinguni_na_kuzimu_wa_vijana_7.htm&sa=U&ei=BFMOVMKIOcfu8AG8qYGwDw&ved=0CBwQFjAC&sig2=_cNQSsg3xPqaEcSedggqVA&usg=AFQjCNEcJrT5MIz9OykyG9OR53nBrPIm9A
Oldest